DK. SHEIN AREJEA NCHINI AKITOKEA INDONESIA

 

Rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dk. Ali mohamed shein, amesema ana matumaini makubwa kwa zanzibar kujiimarisha zaidi katika uwekezaji, utalii na kilimo, kutokana na fursa nyingi zilizotolewa na nchi ya indonesia.

Dk shein ambae amerejea nchini baada ya kukamilisha ziara ya kiserikali ya siku saba nchini indonesia, amesema uwezekano wa zanzibar kupiga hatua zaidi ya kimaendeleo katika sekta hizo upo kwani wawekezaji wa indonesia wameonesha matumaini ya kuja kuwekeza nchini.

Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari ametilia mkazo suala kuimarika kwa sekta ya utalii na kufikia katika kiwango cha juu ambacho kitaongeza pato la taifa kwa kiasi kikubwa.

Kuhusu suala la kilimo cha mwani, dk. Shein amesema ili kukiimarisha kilimo hicho, kinahitaji  kufanyiwa mabadiliko kwa kutumia mbegu za aina mpya ambazo zitaliongezea ubora zao hilo na kuongeza tija kwa wakulima.

Aidha ameeleza kuwa indonesia inataria kuleta ujumbe mkubwa kungalia maeneo ya uwekezaji na namna bora ya kuimarisha sekta ya utalii.