DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMETEKELEZA AHADI YAKE YA KUTOA SHILINGI MILIONI 40

 

 

Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania ,dkt  john pombe magufuli ametekeleza ahadi yake ya kutoa shilingi milioni 40 kuchangia mradi wa samaki unaotekelezwa na kikosi cha jeshi la ulinzi la wananchi wa tanzania (jwtz) kikosi cha 27kj makoko kwa jailli ya kujenga mabwawa mapya kumi kwa nia ya kuuendeleza mradi huo.

Katibu wa rais bwana ngusa samike amemkabidhi fedha hizo kwa mkuu wa kikosi cha 27 kj luteni kanali jaston mshashi kilichopo makoko mkoani mara huku mkuu wa majeshi ,jenerali venance mabeyo akishuhudia tukio hilo.

Mkuu wa majeshi jenerali venance mabeyo amemshukuru rais dkt magufuli kwa kutimiza ahadi yake aliyoitoa september 06,2018 wakati akizindua mradi wa ufugaji wa samaki kwa kutumia mabwawa na mjini musoma na kuongeza kuwa licha ya shughuli ya msingi ya ulinzi na usalama ,jeshi hilo litaendelea kutekeleza kauli mbiu ya rais dkt magufuli ya tanzania ya viwanda.

Aidha mkuu wa kikosi cha 27 kj luteni kanali jaston mshashi amesema fedha zilizotolewa na rais dkt magufuli ni  kutekeleza ahadi yake ya kutoa kiasi cha shilling milioni 40 kwa jailli ya ujenzi wa mabwawa kumi mapya kuunga mkono jitihada za jeshi hilo zitatumiwa kwa matumizi yaliyokusudiwa