Trump kuiondoa nchi yake katika mkataba wa Biashara huria

Rais Mteule wa Marekani Donald Trump amesema ataiondoa nchi yake katika mkataba wa Biashara huria katika eneo la Bahari ya Pasifiki –TPP, mara tu atakapoanza rasmi kutekeleza majukumu yake. Katika ujumbe alioutoa kwa njia ya video akielezea masuala yenye kipaumbele kwake katika siku mia moja za kwanza za urais wa marekani, trump ameuita mkataba huo unaoijumuisha marekani na nchi nyingine kumi na moja za ukanda huo kama ‘janga kwa marekani’. Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe, AMEsema bila Marekani, mkataba huo utakuwa hauna maana tena. Donald Trump ambaye atachukua RASMI MADARAKA tarehe 20 Januari mwakani, wakati wa kampeni yake aliahidi kuiondoa Marekani