DONALD TRUMP KUZURU UFARANSA KWA ZIARA YA SAA 24

Rais wa Marekani Donald Trump yupoziarani nchini Ufaransa kwa ziara ya siku moja ambapo atatumia muda mwingi pamoja mwenyeji wake emmanuel macron.

ziara ya Rais wa Marekani mjini Paris inaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 100 ya kuingia kwa marekani katika vita kuu vya Dunia, na kuanzisha uhusiano kati ya Maraisi hao wawili.

Macron na trump mwanzo uhusiano wao ulikua mgumu mwaka mmoja uliopita. pamoja na kuwa na migogoro kuhusu biashara ya kimataifa na suala la mazingira, ambapo Raisi Donald Trump alijitoa kwenye mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.