DR. SHEIN AMEYAAGIZA MASHIRIKA YA NDEGE YAENDELEE KUSHIKAMANA KATIKA KUIMARISHA HUDUMA ZA UFAFIRI WA ANGA

 

Rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dr. Ali mohamed shein ameyaagiza mashirika ya ndege barani afrika yaendelee kushikamana  katika kuimarisha huduma za ufafiri wa anga kwa lengo la kuifanya  sekta ya utalii barani humo kukua zaidi.Amesema tabia ya kuendelea kuyaachia mashirika ya kigeni kutoa huduma kwa kampuni zinazosafirisha watalii katika mataifa ya afrika inaweza kuviza azma ya afrika katika kuitegemea sekta hiyo kiuchumi.Rais wa zanzibar alitoa kauli hiyo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na makamu wa pili wa rais wa zanzibar balozi seif ali iddi wakati akiufungua mkutano wa saba wa siku tatu wa mashirika ya ndege ya afrika {afraa} unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa zanzibar beach resort mazizini nje kidogo ya mji wa zanzibar.

Alisema usafiri wa anga na utalii ni sekta muhimu kimataifa zinazokuwa kwa haraka kiuchumi na kwenda sambamba katika uendeshaji wake jambo ambalo mataifa ya bara la afrika kupitia taasisi inayosimamia mashirika ya ndege ya afrika {afraa} hayana budi kuhakikisha sekta hizo zinaendelea kujengewa miundombinu madhubuti.Alieleza harakati za usafiri wa anga zinazowaunganisha watalii wanaotembelea maeneo mbali mbali duniani  zinatarajiwa kuongeza mapato ya nchi husika sambamba na fursa za ajira  kwa zaidi ya milioni 400,000,000/-.Alivitolea mfano visiwa vya zanzibar vilivyopiga hatua kubwa kimaendeleo na uchumi katika sekta ya utali kutokana na kuimarika kwa huduma za usafiri wa anga zinazowaunganisha watalii kutoka pambe mbali mbali duniani.Aliyashauri na kuyakumbusha mashirika ya ndege barani afrika  kuongeza juhudi za kuziongezea safari za nje ya bara hilo ili watalii wanaopanga kufanya safari za ndege ndani ya mataifa ya bara hili yatumie ndege zao jambo ambalo litachangia kuongeza mapato.Akitoa taarifa katibu mkuu wa mashirika ya ndege ya afrika {afraa} bwana abdelrahmane berthe alisema muingiliano wa uwajibikaji wa mashirika ya usafiri wa anga afrika katika kutoa huduma zao lazima yaoane ili kuleta tija kwa maeneo yote ya dunia.

Bwana abdelrahmane  alisema soko la utalii linalotarajiwa kuchukuwa nafasi ya kwanza kwa mapato ya uchumi ulimwenguni badala ya mafuta na gesi asilia bado halijafikia lengo.Alieleza kwamba hali hiyo inatokana na baadhi ya maeneo yenye rasilmali za asili kwa biashara ya utalii kutofikiwa na huduma za usafiri wa anga kwa kukosekana kwa miundombinu ya sekta hiyo.Naye makamu wa rais wa  mashirika ya ndege ya afrika bw. Raphael kuuchi alisema takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya dola za kimarekani bilioni 72 zinakusanya  kila mwaka kutoka na biashara ya sekta ya usafiri wa anga barani afrika.Bwana kuuchi alisema kiwango hicho kimekuja kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watalii wanaoingia na kutoka barani afrika.Alifahamisha kwamba mikakati zaidi inahitajika kuwekwa hasa katika mataifa wanachama wa afraa katika kuona nchi hizo hazitawekwa nyuma kwenye biashara ya utalii duniani.Mkutano wa sita wa mashirika ya ndege ya afrika  ulifanyika mwezi mei mwaka 2017 katika mji wa hammamet nchini tunisia ukiwa chini ya ushirikiano na shirika la ndege la nchi hiyo tunisair.