DR. SHEIN KUPONGEZA SERIKALI YA CHINA KATIKA KUIMARISHA MRADI MKUBWA WA MAJI

Rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameanza ziara zake za kikazi katika wilaya zote za zanzibar kuangalia uendelezaji wa miradi ya maendeleo.
Ziara hiyo imeanzia katika wilaya ya kaskazini b unguja na kupongeza serikali ya china katika kuimarisha mradi mkubwa wa maji utakaogharimu dola milioni 5 nukta 5 za marekani ambao kituo kikuu kinajengwa donge mbiji.
Akizungumza na uongozi wa kampuni ya ujenzi wa mradi huo huko kisongoni ameeleza kuwa wananchi wanamatumaini makubwa ya kupata huduma hiyo ya maji mara maada ya kukamilika mradi huo ufadhili wa serikali ya china na unatarajiwa kukamilika julai mwakani.
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya maji zanzibar (zawa), dk. Mustafa ali garu akitoa taarifa ya mradi huo amesema utakuwa na vituo vitano na utanufaisha vijiji vya donge, kisongoni, chaani, kwa upande wa kaskazini unguja na miwani, kiboje kwa mkoa wa kusini.
Awali dk. Shein amepokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya mkoa huo wa kaskazini unguja iliyosomwa na mkuu wa mkoa huo vuai mwinyi mohammed alieleza mafanikio yaliopatikana katika sekta za maendeleo kwa wakaazi wa mkoa huo ikiwemo kilimo, na utalii.
Hata hivyo ameeleza kuwa bado hali ya udhalilishaji wa wanawake na watoto katika mkoa huo si ya kuridhisha kwa vile matukio hayo yanaendelea kutokea mara kwa mara.
Dkt shein katika ziara hiyo alipata fursa ya kuzungumza na wananchi aliwaeleza kuwa ziara hiyo inathibitisha jinsi utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020 huku akisisitiza viongozi kuangalia harakati za maendeleo katika maeneo ya wananchi badala ya kukaa ofisini.
Katika ziara hiyo dkt shein pia ametembelea kiwanda cha sukari mahonda ambapo meneja wa mradi wa kiwanda hicho tushar mehta amesema uzalishaji wa sukari umeongezwa kutoka kukamua tani 400 za miwa kwa siku hadi tani 800 za miwa kwa siku na kinaweza kufikia tani 1250 kwa siku.
Rais wa zanzibar pia amefungua tawi la ccm la kitope b, na kupongeza hatua hizo zilizochukuliwa na wana ccm kujenga tawi litakalosaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha chama hicho.