DR. SIRA AAGIZA KUFANYIKA KIAKO CHA PAMOJA KATI YA MAMLAKA YA USAFIRI BAHARINI ZANZIBAR NA SHIRIKA LA BANDARI

waziri wa ujenzi, mawasiliano na usafirishaji dk. sira ubwa mamboya ameagiza kufanyika kiako cha pamoja kati ya mamlaka ya usafiri baharini zanzibar na shirika la bandari kuangalia namna watakavyoiondosha meli iliyokata nanga na kupotelea katika bahari ya mangapwani.
meli hiyo inayomilikiwa na kampuni ya jack enterprises imekata tanga katika bandari ya malindi tokea mwanzoni mwa mwezi januari imekuwa ikilalamikiwa na wamiliki wa hoteli iliyopo karibu na bahari hiyo kwa hofu ya kuleta madhara wakati maji yanapojaa.
waziri huyo ambae amefika eneo hilo kuangalia meli hiyo alipata maelezo kutoka kwa mkaguzi wa meli wa zma said shaib is-haq amesema kabla ya hatua ya kuiondosha taasisi hizo ziwafikiane juu ya gharama zitakazotumika katika kuirejesha eneo la bandari ya malindi.
mwanasheria kutoka mamlaka ya usafiri baharini zanzibar amesema mbali na meli hiyo kuwa kero katika eneo hilo kiusalama pia haikubaliki kuwepo eneo hilo.