DRC HAINA FEDHA ZA UCHAGUZI WA RAIS

Waziri wa fedha na bajeti nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, amesema kwamba nchi yake haitaweza kutafuta fedha kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa rais mwaka huu.
Rais Joseph Kabila alikwisha maliza muhula wake kama rais wa nchi hiyo mnamo December mwaka wa jana.Makubaliano baina ya pande mbili, upande wa upinzani na serikali iliyoko madarakani kwa pamoja walikubaliana kuwa uchaguzi huo ungefanyika mwishoni mwa mwaka huu wa 2017.
Ingawa waziri huyo Pierre Kangudia, amesema kwamba kwa muujibu wa tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwamba uchaguzi huo gharama yake ni dola bilioni moja nukta nane zikiwa ni fedha za maandalizi ya uchaguzi na uchaguzi wenyewe, na kusema kwamba serikali yake haitaweza kumudu gharama hizo.
Wapinzani wa rais Joseph Kabila, wapinzani mara kwa mara wamekuwa wakimtuhumu kwa kurejelea kuchelewesha uchaguzi kwa lengo la kusalia madarakani