EKARI MIA TATU ZA MIKOKO YA FUKWE YA KISAKASAKA ZIMEHARIBIWA

Zaidi ya ekari mia tatu za mikoko ya fukwe ya kisakasaka zimeharibiwa kwa shughuli za kijamii hali inayohatarisha mazingira ya fukwe katika eneo hilo.
Tatizo hilo linadaiwa kuchangiwa na idadi kubwa ya watu wa kijiji hicho pamoja na vijana kutegemea rasilimali ya misitu kwa shughuli za kijamii.
Katibu wa jumuiya ya upandaji na uhifadhi wa mikoko kisakasaka jumsika khatibu ali vuai amesema baada ya kubaini athari za kimazingira kijijini humo wameamua kuhifadhi mikoko na tayari ekari 20 zimeshapandwa miti elfu tatu na tayari jamii imeanza kupata mwamko wa kupanda miti hiyo
Baadhi ya wakaazi wa kijiji hicho wakizungumza katika kikao cha kujadili mabadiliko ya tabia nchi na athari zake naibu sheha wa shehia ya kombeni ali vuai kassim amesema wamekuwa wakichukuwa hatua kadhaa kwa wanaoharibu mikoko kwa kutumia kanuni ndogo walizoziweka.
Kikao hicho ni sehemu ya mafunzo kwa jumuiya hiyo
Yanayotolewa kupitia mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabia nchi ambapo afisa wa mradi huo zanzibar salim bakar amesema lengo ni kushajihisha wananchi kusaidia kuimarisha mazingira kwa faida yao