ELIMU YA URAIA INAMJENGA MTU KUJIAMINI NA KUFAHAMU HAKI

 

 

kituo cha huduma za sheria    zanzibar kimesema elimu ya uraia inamjenga mtu kujiamini na kufahamu haki zake za msingi pamoja na kufuata sheria za nchi  .

akizungumza katika mafunzo ya elimu ya uraia kwa walimu wa skuli za msingi na sekondari mkoa wa kusini unguja afisa mipango wa kituo cha huduma za sheria    ali haji amesema  iwapo walimu watayafanyia kazi mafunzo hayo katika ufundishaji yatamjenga mwanafunzi kuwa raia mwema katika kushirikii vizuri kazi za kujenga taifa

amefahamisha kuwa muonekano wakuifahamu elimu hiyo umekuwa mdogo katika jamii na kusababisha kufanyika kwa makosa mbalimbali   yasiyotegemewa.

walimu walioshiriki mafunzo hayo wamesema  wananchi wengi wanatatizo la kutoifahamu elimu ya  uraia hivyo mafunzo hayo yatawasaidia katika kujenga jamii bora .