ENEO LILILOKUSUDIWA KUJENGWA HOSPITALI YA MKOA LISITUMIKE KWA MATUMIZI MENGINE.

 

 

Kaimu mkuu wa mkoa wa kusini unguja  mhe; idrissa kitwana mustafa amesema serikali mkoani humo italilinda eneo la binguni uwanja wa ndege lililokusudiwa kujengwa hospitali ya  mkoa huo lisitumike kwa matumizi mengine.

Mhe, kitwana ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kulikagua eneo hilo akiwa na viongozi na watendaji mbali mbali wa serikali pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo.

Amesema amri hiyo ilitolewa na rais wa zanzibar dr ali moh’d shein baada ya kuona ujenzi unaendelea katika eneo hilo hivyo aliutaka uongozi wa mkoa kusimamisha ujenzi huo.

Nae mkuu wa wilaya ya kati ndugu mashavu saidi sukwa ameutaka uongozi wa wizara ya afya kufuatilia kwa karibu maendeleo ya eneo hilo ili serikali iweze kutimiza azma ya ujenzi wa hospitali hiyo kama ilivyokusudiwa.