ETHIOPIA KUISHIWA NA CHAKULA IFIKAPO MWEZI UJAO

Umoja wa mataifa umesema huenda ethiopia inatarajiwa kuishiwa na chakula cha dharura kwa watu milioni 7 nukta 8 wanaokabiliwa na ukame mwishoni mwa mwezi huu .
Taarifa zinadai kuwa serikali ya nchi hiyo bado haina pesa za kuendelea kutatua tatizo hilo peke yake baada ya kutenga dola milioni 381 katika miaka miwili iliyopita.
Mashirika ya kutoa misaada na serikali yametoa wito wa msaada zaidi licha ya hofu ya kutokea majanga mengine duniani.