EVERTON ROMELU LUKAKU AMEKATAA KANDARASI

 

 

Mshambuliaji wa everton romelu lukaku amekataa kandarasi yenye faida kubwa kwake katika historia ya klabu hiyo.

Klabu hiyo ya ligi ya Uingereza ilikuwa na matumaini kwamba mchezaji huyo wa Ubelgiji ataongoza kandarasi ya miaka mitano inayoaminika kugharimu pauni 140,000 kwa wiki.

Msemaji  wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, Mino Raiola amesema kwamba kunauwezekano wa asilimia 99.9 kusaini kandarasi mpya katika uwanja wa Goodison Park.

Ingawa  Lukaku amesema  kwamba hana mpango wa kuongeza kandarasi ambayo imesalia miaka miwili kukamilika.

Lukaku hajaficha kuhusu mpango wake wa  kusakata soka katika  timu  bingwa Ulaya na amehusishwa na uhamisho wa kurudi katika klabu yake ya zamani  ya  Chelsea, ambapo alijiunga na Everton kwa kitita cha pauni milioni 28 mwaka 2014.

Ombi la kandarasi ya Everton bado lipo wazi huku klabu hiyo ikisema kuwa majadiliano zaidi huenda yakapata makubaliano.

Kwa sasa  Lukaku hajakubali kandarasi yoyote na Everton  na huenda ikaitisha kitita cha pauni milioni 60 kwa mchezaji huyo aliyefunga mabao 19 msimu huu.