FAMILIA YA WATU SITA IMEKOSA MAKAAZI

Familia ya watu sita imekosa makaazi baada ya nyumba zao kufauati mmong’onyoko wa ardhi katika shehia ya ng’ombeni kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha.
Familia hizo ni za bi fatma abeid na juma atosha ambapo katika tukio hilo mtoto ali abdillahi miaka 15 amejeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta na amelazwa katika hospitali ya abdallah mzee mkoani.
Mkuu wa wilaya ya mkoani hemed suleiman abdallah ametoa pole kwa familia zilopatwa maafa hayo na kuwataka wananchi kutojenga katika maeneo ya milima na njia za maji, kwani si salama hasa katika kipindi cha mvua.
Amesema serikali ya wilaya itachukuwa juhudi za kuwapatia makaazi familia hiyo.