FAMILIA ZENYE KULEA WATOTO YATIMA WAMEKABIDHIWA KADI YA BIMA YA AFYA YA MFUKO WA NHF

 

 

 

Familia zenye kulea watoto yatima  hamsini wa shehia tatu za tumbatu wamekabidhiwa kadi ya bima ya afya ya mfuko wa nhf ili  waweze kupata matibabu kwa urahisi na bila usumbufu .

Familia hizo ambazo kipato chao ni cha hali ya chini wamepatiwa kadi hizo ili kuwapunguzia gharama za matibabu na dawa ambazo hapo awali   walishindwa kuzipata kwa urahisi.Wakizungumza na zbc wananchi hao wamesema  kadi  zilivyotolewa kwa watoto hao zimeleta unafuu kwao na kuwapunguzia gharama ya ukali wa maisha kutokana na kuwa  watoto hao wanaishi bila ya wazazi wao .

Mkurugenzi wa kijiji cha sos bi  asha .amewataka walezi wa watoto hao   kusimamia vyema majukumu ya ulezi, kwa kuwapatia elimu,  huku wakizingatia umuhimu wa kuwahimiza watoto wao kudumisha usafi wa mwili  ili kujikinga  na maradhi mbalimbali.Aidha bi asha amesema azma ya sos ni kuwafikia watoto mia nne kwa mwaka 2017/2018, kupitia  mradi wa malezi mbadala unahudumikia watoto hao hamsini

Nae  afisa wa mfuko wa nhf  luck  chaula, amesema kuwa kadi hiyo itawezesha kupata matibabu popote pale na itamrahisishia mzazi kupata matibabu hata mkama hana fedha.Kwa upande wake afisa mradi bi  nyezuma simai, amesema malengo ya mradi huo ni kuzifikia familia zenye mazingira magumu kwa kuwajengea uwezo katika nyanja ya elimu na afya na kufanya hivyo kutapunguza msongamano  wa watoto  wanaofika katika kituo cha sos  kwa ajili ya malezi