FAWE WAMEWEKA MKAZO KUHAKIKISHA MTOTO WA KIKE ANATAMBULIKANA KITAALUMA

Jumuiya ya kumuendeleza kielimu mtoto wa kike zanzibar fawe, imesema kuwa kuwashirikisha wanafunzi wa kike katika sherehe za arusi, kumewasababishia wengi wao kutofaulu vyema katika masomo yao.
Akifungua mafunzo kwa walimu wanaosomesha somo la sayansi kwa skuli kumi za zanzibar zenye klabu za mradi wa stem, mwenyekiti wa fawe, bi mwatima abdalla juma, amesema baadhi ya wazazi wanashindwa kuwahimiza watoto wao kushulikia masomo na kuwaacha kujishughulisha na mambo ya kifamilia, huku wakisahau umuhimu wa kupata elimu.
Hivyo amewataka walimu hao kusimamia kwa umakini usomeshaji wa somo la sayansi kwani taifa linatarajia kupata wataalamu bora wa fani mbali mbali ikwemo madaktari na wahandisi.
Mratibu wa fawe bi hinda abdalla ajmiy, amesema wameweka mkazo kuhakikisha kuwa mtoto wa kike anatambulikana kitaaluma kupitia somo la sayansi, kwa vile tayari wanafunzi wanaodhaminiwa na fawe wameonesha muelekea mzuri.
Katika mafunzo hayo wanafunzi wa klabu ya stem kutoka skuli ya mikindani dole, wameonesha kazi za uhandisi wa ujenzi, ufundi wa umeme na fani ya udaktari, na kuelezea matarajio yao.