FEDHA ZAHITAJIKA ILI KUKAMILISHA ENEO LA MRADI WA JAMII WA KILIMO CHA MPUNGA PADEP TWO, HUKO CHEJU

 

Jumla ya shilingi milioni mia moja na kumi na tisa zinahitajika ili kukamilisha eneo la mradi wa jamii wa kilimo cha mpunga padep two, katika bonde la cheju.

Wakulima wa bonde la cheju, wamesema iwapo watapata fedha hizo wataweza kuondokana na matatizo yanazowakabili ikiwemo kuchimba kisima na kuimarisha huduma za miundo mbinu za umwagiliaji jambo ambalo watafanikiwa kwa kiasi kikubwa katika uzalishaji wa chakula.

Hayo yamebainika wakati wakulima hao wakitoa maelezo kwa mshauri wa rais masuala ya kimataifa fedha na uchumi, balozi mohamed ramia aliyefika katika bonde hilo kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya wakulima wa kilimo cha mpunga kwa msimu huu.

Akizungumza na wakulima hao, balozi ramia ameelezea kuridhishwa na jitihada wanazochukua za kuimarisha kilimo na kuwataka kuongeza juhudi zaidi za uzalishaji ili zanzibar iweze kuondokana na uagizaji wa chakula nje ya nchi.