GARI LAGONGA WATU KADHAA LONDON

Mtu mmoja ameuawa na wengine wanane kujeruhiwa baada ya gari kugonga umati wa watu waliokuwa wakitembea karibu na msikiti kaskazini mwa london.
Polisi wa kupambana na ugaidi wako eneo la tukio huku wakilielezea tukio hilo kama ni la kigaidi.
Waziri mkuu theresa may amesema tukio hilo ni kusikitisha na kuwapa pole waathirika wote wa tukio hilo.
Baraza kuu la waislamu nchini uingereza limesema kuwa walengwa wa tukio hilo walikuwa ni waumini, huku majeruhi wengi wakiaminika kuwa ni wale waliokuwa wamemaliza swala ya jioni.
Tayari mtu moja amekamatwa kufuatia shambulio hilo lililotokea katika wilaya ya finsbury park.