GARI ZA ABIRIA BUBUBU MAGENGENI ZINASHINDWA KUTUMIA NJIA HIYO KUTOKANA NA KUHARIBIKA VIBAYA

 

Gari za abiria zinazotumia  njia ya bububu magengeni hadi mwanyanya zinashindwa kutumia njia hiyo kutokana na kuharibika vibaya kwa  kuwa na mashimo mengi hivi sasa.Kufuatia hali hiyo wananchi wanapata usumbufu mkubwa na kulazimika kutembea kwa miguuu au vyombo  vidogo vidogo hadi barabara kuu.

Wananchi hao wameiambia zbc kuwa  pamoja na jitihada za kutafuta  gari nyengine zitakazoweza kusaidia  abiria wa njia hiyo   wameshindwa  kufanikiwa  baada ya madereva kukataa  kuitumia njia hiyo kwa muda huu.Wamesema   kwa kuwa  wamekuwa wakitembea masafa marefu kufuata huduma   muhimu wamewaomba viongozi wa jimbo waliowachagua na  baraza la manispaa kuwasaidia kuondokana na tatizo hilo.Wamesema ni vyema serikali kuifanyia marekebisho mapema  barabara   hiyo ili kuepuka hasara ya gharama kubwa ya kuijenge upya.