HAKUNA MWANANCHI ATAKAESALIMIKA KUSAFIRISHA KARAFUU KUTOKA SHEHIA MOJA KWENDA NYENGINE BILA YA KUWA NA KIBALI

Mkuu wa mkoa wa kaskazini pemba mhe omar khamis othman amesema hakuna mwananchi ambaye atasalimika iwapo atakwenda kinyume na sheria kwa kusafirisha karafuu kutoka shehia moja kwenda nyengine bila ya kuwa na kibali kilichoainishwa kisheria .
Akizungumza na zbc mh omar amesema kwa mujibu wa sheria ya karafuu ni kosa kusafirisha karafuu kutoka shehia moja kwenda nyengine bila ya kuwa na kibalia ambacho kinatambulika kisheria na ambacho kinataolewa na sheha .
Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo baada ya vyombo vya ulinzi kufanikiwa kumkamata kijana mbarouk salim bakar ambaye alikuwa anasafirisha karafuu kutoka wilaya ya wete kwenda chake chake bila ya kuwa na kibali cha kusafirishia .
Mapema mkuu wa wilaya ya wete rashid hadid rashid na kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini pemba kamishna msaidizi haji khamis haji amesema kijana huyo amekamatwa kutokana na kukaidi agizo la kukata kibali kutoka kwa sheha
Katika utetezi wake kijana huyo amesema amepanga kukata cheti shehia nyengine kwani sheha wa shehia ya piki akimlazimisha kuuza karafuu kwenye vituo vya zstc wilaya hiyo na sio wilaya nyengine.