HALI SIO YA KAWAIDA KWA MSHAMBULIAJI WA MANCHESTER UNITED ROMELU LUKAKU,

 

Hali sio ya kawaida kama ilivyokuwa  hapo mwanzo kwa mshambuliaji wa manchester united romelu lukaku, kwani baada ya kufunga sana  siku hizi amekuwa akisuasua na  kucheka na nyavu za wapinzani.

Majanga mapya yameibuka kuhusiana na Romelu Lukaku kwani sasa anaweza kukabiliwa na kifungo cha hadi mechi tatu.

Video za marudio zinaonesha Lukaku akimpiga teke mlinzi wa Brighton Gaetan Bong mara mbili. Muamuzi wa mchezo huo atawasilisha ripoti ya mchezo huo hii leo na kama Lukaku atakutwa na hatia ataadhibiwa.

Endapo Lukaku atapewa adhabu hiyo atazikosa mechi mbili kubwa zijazo ambapo kwanza atawakosa Arsenal na kisha wiki baada ya Arsenal hatakuwepo wakati United wakiikabili Manchester City.