HALI YA KUTATANISHA INAENDELEA NCHINI ZIMBABWE

Hali ya kutatanisha inaendelea nchini zimbabwe wakati kukiwa na mazungumzo ya kimyakimya ya kuutatua msukosuko wa kisiasa wa nchi hiyo na kuangalia uwezekano wa kumalizika kwa utawala wa miongo minne wa rais robert mugabe.

Mugabe yuko kwenye kizuizi cha jeshi na hakuna dalili ya kuonekana   katika wakati huu ambapo wanajeshi bado wanashika doria katika mitaa ya mji mkuu, Harare, huku wasiwasi ukiendelea kutanda.

Maafisa kutoka jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa afrika – sadc wamekutana leo katika mji mkuu wa botswana, gaberone kuujadili mgogoro huo, wakati Rais wa afrika kusini Jacob Zuma amewatuma wajumbe wake mjini harare kukutana na jeshi.

Kasisi mmoja wa kanisa katoliki anaongoza mazungumzo ya uwezekano wa kujiuzulu rais robert mugabe, ijapokuwa   anasisitiza kuwa anaweza kuondolewa kupitia uchaguzi wa uongozi wa chama chake cha zanu-pf.

Wakati huo huo kiongozi wa upinzani morgan tsvangirai, ambaye amekuwa akipokea matibabu ya maradhi ya saratani nje ya zimbabwe, amerejea harare hapo jana.