HALI YA MARADHI YA KIPINDUPINDU BADO SI YA KURIDHISHA

Hali ya maradhi ya kipindupindu bado si ya kuridhisha na kusababisha wizara ya afya kufungua kambi ya dharura katika kijiji cha gamba.
Akizungumza baada ya kupokea vitanda vya kulaza wagonjwa wa kipindupindu vilivyotolewa na unicef mkururugenzi wa kinga na elimu ya afya dk. Mohamed fadhili amesema tangu serikali itangaze kuwepo kwa maradhi hayo kambi ya chumbuni imeshatibu wagonjwa 180 ambapo mtu mmoja amefariki dunia.
Amesema kambi ya gamba nayo imelaza wagonjwa ishirini huku kambi ya chumbuni imekuwa ikiendelea kupokea wagonjwa na kuwataka wananchi kutii agizo linalokataza kufanya biashara ili kuepusha athari za afya.
Amefahamisha kuwa wagonjwa wengi wanaopokelewa katika kambi ya chumbuni ni kutoka maeneo ya awali yaliyoanza kuripotiwa ugonjwa huo.
Wakati huo huo waziri wa afya mh mahmood thabiti kombo amepokea vitanda na kutembelea wagonjwa waliolazwa katika kambi ya chumbuni.