HALI YA VITENDO VYA UDHALILISHAJI KWA WATOTO ZANZIBAR BADO IKO JUU

 

Wadau wa masuala ya ufuatiliaji wa vitendo vya udhalilishaji wamesema licha ya .kuwepo kwa sheria mbali mbali lakini bado wafanyaji wa matukio hayo wamekuwa hawana woga.Wamesema  hali ya vitendo vya udhalilishaji kwa watoto zanzibar bado iko juu na imekuwa ikirudisha nyuma utendaji   wao wa kazi, hatua ambayo imewapelekea wadau hao kujadiliana namna bora ya kuiwezesha sheria iliopo iweze kufanya kazi zaidi.

Mkufunzi kutoka taasisi ya (c sema) inayoshughulikia masuala ya watoto tanzania bara na zanzibar kwa kushirikiana na sos nd. Michael kehongoh, amesema sera za utekelezaji katika huduma za watoto  na ufuatiliaji kwa jumla imeonekana upo chini  hivyo kuna  haja ya kufanya mapitio ya sera  ili iweze kuwadhibiti wahalifu.Aidha  ameiomba serikali kuziwezesha taasisi zinazoshulikia masuala ya udhalilishaji, ili ziweze kutekeleza kazi zao za ufuatiliaji wa vitendo hivyo kwa ufanisi.

Nae mratibu wa malezi na makuzi ya watoto kutoka sos bi. Nyezuma ismail issa, amesema tatizo la udhalilishaji wa watoto limekuwa likiwaweka wazazi katika wakati mgumu kutokana na kuripotiwa kwa wingi matendo hayo na kutojua hatma ya watoto.   Diwani wa wadi ya tumabatu kona juma ali,.amesema kuna umuhimu kwa wazazi kuwalinda watoto ili kuwaepusha na vitendo hatarishi vinavyojitokeza katika jamii