HALMASHAURI (NEC) YA CHAMA CHA MAPINDUZI IMEMTEUA DK. BASHIRU ALI KAKURWA KUWA KATIBU MKUU WA CCM.

 

halmashauri kuu ya taifa (nec) ya chama cha mapinduzi  (ccm), imemteua aliyekuwa mwenyekiti wa tume maalum ya kuchunguza mali za chama hicho dk. bashiru ali kakurwa kuwa katibu mkuu wa ccm.mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (ccm) taifa na rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania dk. john pombe magufuli alilitangaza jina la dk. bashiru kumrithi katibu mkuu mstaafu wa chama hicho abdulrahman kinana baada ya kupitishwa na nec katika vikao vilivyomaliza hapo jana.bashiru alikuwa ni mwenyekiti wa tume ya kufuatilia mali za ccm iliyoundwa na mwenyekiti huyo wa ccm ambaye jina lake lilitangazwa mbele ya kikao cha halmashauri kuu ya taifa ya ccm (nec) na hatimae wajumbe hao waliridhia kwa pamoja.tukio hilo limetokea katika kikao cha halmashauri kuu ya ccm taifa (nec) kilichoendelea katika ukumbi wa mikutano ikulu jijini dar-es-salaam ambapo rais magufuli pia, alikabidhiwa ripoti kutoka kwa kamati ya kufuatilia mali za ccm aliyoinda.katika maelezo yake, rais magufuli alipongeza kazi kubwa iliyofanywa na kamati hiyo ambayo iliwasilisha ripoti yake katika kikao hicho cha nec na kumpongeza mwenyekiti wake ambaye amepata wadhifa huo wa kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa ccm taifa.nae rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi ambaye pia ni makamo mwenyekiti wa ccm zanzibar dk. ali mohamed shein alimpongeza katibu mkuu huyo mpya pamoja na kuipongeza tume hiyo kwa kazi nzuri iliyofanya ndani ya miezi mitano.sambamba na hayo, kikao hicho kiliyapitisha majina ya makatibu wakuu wa jumuiya za ccm ambapo kwa upande wa jumuiya ya vijana (uvccm) aliyechaguliwa kuwa katibu mkuu ni raymond mwangala, jumuiya ya wazazi katibu mkuu ni erasto sima na jumuiya ya wanawake ni queen mlozi ambaye ni mkuu wa wilaya ya tabora.

wakati huo huo rais magufuli alifanya futari maalum katika ukumbi wa ikulu jijini dar-es-salaam ambapo katika maelezo yake baada ya futari hiyo, rais magufuli alitoa shukurani kwa wageni wote waliohudhuria katika futari aliyowaandalia hapo  wakiwemo viongozi mbali mbali wa dini, chama, serikali pamoja na wananchi wa mkoa wa dar-es-salaam.aidha, rais magufuli alitumia fursa hiyo kueleza kuwa mwezi wa ramadhani ni mwezi wenye heshima kwa watu wa dini zote hasa ikizingatiwa kwua mwezi huo ni mwezi wa toba.

Rais magufuli aliwasisitiza waislamu kuendelea kuliombea taifa ili liwe na amani na upendo pamoja na kuziombea serikali zote mbili ili yale yote yaliopangwa na serikali hizo yaweze kufanikiwa kwani mwezi wa ramadhani maombi hukubalika kwa haraka.pamoja na hayo, alitoa shukurani kwa waziri anayeshughulikia masuala ya dini ya kiislamu kutoka nchini saud arabia dk. saleh abdul aziz, kwa uwamuzi wake wa kuiunga mkono tanzania katika kuimarisha sekta ya elimu na kueleza azma ya nchi hiyo ya kutaka kujenga chuo kikuu cha kiislamu hapa tanzania.nae waziri huyo wa masuala ya dini kutoka saud arabia alizipongeza juhudi zinazochukuliwa na serikali ya jamhuri ya tanzania chini ya uongozi wa rais dk. john pombe magufuli na kuahidi kuwa serikali yake itaendelea kuiunga mkono tanzania ili maendeleo zaidi yaweze kufikiwa.kiongozi huyo alimpongeza rais magufuli kwa kuwaweka wananchi wa tanzania kuwa wenye umoja na mshikamano hali ambayo imepelekea tanzania kuendelea kuimarika kiuchumi na kupata maendeleo makubwa.