HALMASHAURI YA KASKAZINI B INATARAJIA KUBORESHA NA KUANZISHA VYANZO VIPYA VYA MAPATO

Halmashauri ya wilaya ya kaskazini b inatarajia kuboresha na kuanzisha vyanzo vipya vya mapato katika maene nane ili kuongeza mapato na kutoa huduma bora kwa jamii
Akizungumza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji masheha na madiwani mwanasheria wa halmashauri ya wilaya hiyo asya muhammed mzee amesema mpango huo ni kwa mujibu wa kifungu cha sabini cha sheria namba saba ya mwaka 2014 ya serikali za mitaa ambayo inatoa fursa kwa halmashauri kuongeza vyanzo vipya vya mapato
Amesema miongoni mwa vyanzo hivyo ni pamoja na mabadiliko ya vyeti vya mazao ambavyo vitauzwa kwa bei ya shilingi laki mbili na elfu hamsini pamoja na kuwepo kwa makusanyo ya wafanya biashara ndogondogo.
Washiriki wa mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yamewasaidia kuwapa uelewa wa sheria mbalimbali ambazo zitawasaidia katika utekelezaji wa kazi zao kati ya masheha na madiwani
Mkuu wa wilaya ya kaskazini b issa juma ali ameitaka halmashauri kuunda kamati ya kushughulikia ujenzi ili kuondoa usumbufu kwa madiwani na masheha kwa wananchi wao