HALMASHAURI YA WILAYA KATI IMESIMAMISHA NA KUVUNJA UJENZI WA UKUTA

 

Halmashauri ya wilaya kati  imesimamisha na kuvunja  ujenzi wa vikuta unaoendelea  katika mzunguko wa barabara ya njia mbili  kuelekea unguja unguu makunduchi kufutia ujenzi huo kukiuka utaratibu  uliopo.Akizungumza  katika zoezi hilo la uvunjaji afisa majezi wa wilaya ya kati bw, ali abasi vuai amesema uamuzi huo umechukuliwa baada ya mjenzi  huyo kukiuka taratibu za kisheria zilizopo na kuamua kujenga bila ya kibali

Amesema ujenzi huo unaweza kuhatarisha maisha ya watu wanaotumia barabara hizo kutokana na kujengwa bila ya kuwa na vigezo vinavyokubalika kitaalaam.Mwanasheria kutoka halmashauri ya wilaya ya kati nd, othmani nzori  amesema katika ufuatiliaji wao wamegundua kuwa ujenzi huo unafanywa na mwekezaji mmoja wa hoteli ya dow in  iliyopo paje na walipomuita kwa ajili ya maelezo alishindwa kuitikia wito ndipo halmashauri  ikachukua uamuzi huo kisheria

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya kati nd, mohamed salum mohamed   amesema halmashauri inafanyakazi zake kwa kufata utaratibu na sheria zilizopo hivyo haitamfumbia macho mtu yeyote atakae kwenda kinyume na taratibu hizo aidha amepiga marufuku  kwa  wawekezaji na watu mbalimbali kuacha tabia ya kujenga kiholela pasipo kufuata utaratibu uliowekwa ili kuepuka usumbufu na hasara zitakazotokea dhidi yao.