HALMASHAURI YA YA WILAYA YA KASKAZINI ‘A’UNGUJA KUVUKA MAKADIRIO ILIYOJIPANGIA

 

 

Zaidi ya shiliingi  milioni   mia tano  na hamsini na tisa  sawa  na asilimia  miambili  zimekusanywa  na  halmashauri ya  ya wilaya ya kaskazini  ‘a’ unguja  na kuvuka makadirio iliyojipangia, kupitia vyanzo   vyake vya mapato  na  ukusanyaji wa kodi  mbali mbali.

Akiwasilisha taarifa ya mapato  robo  ya tatu  ya mwaka wa fedha 2017/2018  mhasibu mkuu wa halmashauri hiyo, nd. Swaleh  bakari  khamis,  amesema kiwango hicho  ni kikubwa  tafauti na makadirio  waliyojiwekea ya  kukusanya   shilingi milioni 401,693,509,00 ya makusanyo yake.

Amesema mapato hayo yametokana na kodi za maduka, hoteli za kitalii na vyanzo vyengine vya mapato vilivyomo katika wilaya hiyo.

Aidha afisa uendeshaji  wa halmashauri hiyo fakih kombo fakih, amesema  mafanikio hayo ya kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato unatokana na uwajikaji na uaminifu wa watendaji katika kudhibiti ukusanyaji wa mapato.

Mkuurugenzi   wa hamashauri  ya wilaya  ya kaskazini  ‘a’  nd. Mussa ali  makame, amesema halmashauri  imejipanga kuimarisha sekta ya  mifugo, kilimo na uvuvi katika maeneo yao ambayo imeonekana kuwa na kiwango kikubwa cha mapato.

Wanayofanyia kazi pamoja na kuhimiza kuongeza uwajibikaji wa kiutendaji wa kazi zao.

Baadhi  ya madiwani wametoa michango mbali mbali  kuhusiana na  bajeti ambayo imewaridhisha  na kusema mashirikiano mazuri ndio yaliyofanikisha  ukusanyaji mzuri wa mapato hayo.

Kikao hicho cha baraza ya madiwani kimeongozwa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo nd hassan mcha hassan   na kuhimiza  uwajibikaji wenye ufanisi kwa watendaji wa halmashauri hiyo