HASARA INAYOTOKANA NA KUDORORA KWA BIASHARA YA KUKU

 

Wafanya biashara wa kuku katika soko la manzese jijini dar es salaam wameelezea hasara inayotokana na kudorora kwa biashara hiyo.

Wakizungumza na zbc baadhi ya wafanya biashara hao wamesema katika kipindi fulani hukumbwa na hasara inapotokea idadi ya kuku kufa kutokana na kukaa kwa muda mrefu.

Aidha wameelezea nafasi ya soko kwa kuku wa kienyeji kutokana na watu wanavyopendelea kuku hao tofauti na wale wa kisasa.