HATUA YA KUACHILIWA HURU MMOJA WA VIONGOZI MKUU WA UPINZANI VENEZUELA

Rais wa venezuela nicolás maduro amepongeza hatua ya kuachilia huru mmoja wa viongozi wakuu wa upinzani nchini humo leopoldo lopez.
Lopez anaendelea na kifungo cha nyumbani baada ya kukaa gereza kwa zaidi ya miaka mitatu kutumikia kifungo cha miaka 14 kwa tuhuma za uchochezi na ghasia wakati wa maandamano ya kuipinga serikali mwaka 2014.
Rais maduro amesema anaunga mkono na kuheshimu uamuzi wa mahakama lakini amesisitiza suala la kuwepo amani lakini lopez muda mfupi baada ya kuachiliwa amewasisitiza wafuasia wake kuendelea kuandamana barabarani kumpinga maduro.