HATUA YA UTAALAMU WA UTUMIAJI WA TEKNOLOJIA YA KICHINA YA KULIMA MPUNGA ITASAIDIA UZALISHAJI WA MPUNGA ZANZIBAR.

 

Makamu wa pili wa rais balozi seif ali iddi, amesema hatua iliyoanzishwa ya utaalamu wa utumiaji wa teknolojia ya kichina ya kulima na kukuza kilimo cha mpunga itasaidia uzalishaji wa mpunga zanzibar.Akizungumza katika uzinduzi wa utowaji wa mafunzo ya teknolojia hiyo kwa niaba ya makamu wa pili wa rais, waziri wa ofisi ya makamu wa pili wa rais mh. Mohamed aboud amesema hatua hiyo itaweza kusaidia kupunguza uagizaji wa mcele nje ya nchi.Mh. Aboud amesema ni vyema wakulima kutumia teknologia hiyo waliyopewa ili kufikia malengo ya serikali ya mapinduzi ya zanzibar katika kupinguza umasikini.Aidha ameitaka wizara ya kilimo maliasili mifugo na uvuvi kuongeza juhudi za kutafuta washirika wengine wa maendeleo ili kuunga mkono na kuongeza eneo la umwagiliaji maji kwa lengo la kukifanya kilimo hicho kuwa si cha umwagiliaji maji.

Balozi mdogo wa china nchini tanzania bi wang ke, amesema serikali ya china itaendelea kusaidia zanzibar kupitia sekta mbali mbali ikiwemo ya kilimo na kuweza kujitosheleza kwa chakula pamoja na kuwapatia wakulima elimu ya kilimo cha kisasa na kuondokana na kutumia kilimo cha zamani.Katika uzinduzi huo  waziri wa kilimo maliasili mifugo na uvuvi mh. Rashid ali juma, amepata fursa ya kuzungumza na wakulima na kuahidi kuwa wizara yake itahakikisha teknolojia hiyo mpya ya utumiaji wa kilimo cha mpunga kutoka china inawafikia wakulima wote wa unguja na pemba na kuhakikisha mabadiliko yanapatikana katika sekta ya kilimo.Akitoa shukurani kwa niaba ya wakulima wenzake mzee golo, amesema eneo la cheju lina hekari 3000 ambazo kwa sasa bado matumizi yake ni madogo ukilinganisha na ukubwa wa eneo hilo na kuiomba serikali kuhakikisha  eneo hilo liweze  kufanyiwa kazi.Katika hatua nyengine balozi mdogo wa china  bi wang amekabidhi vifaa 32 vya kilimo vikiwemo vya umwagiliaji maji .