HATUA ZA KISHERA KWA SKULI ZA BINAFSI ZITAKAYOBAINIKA KUWACHUJA WANAFUNZI

 

Wizara ya elimu na mafunzo ya amali zanzibar imesema itachukua hatua za kishera kwa skuli za binafsi zitakayobainika kuwachuja wanafunzi wake wa  kidato cha nne wasiofikia kiwango cha ufaulu kilichowekwa.

Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya amali mh. Mmanga mjengo, amesema serikali haikubaliani na utaratibu huo ambao ni kinyume na taratibu na sheria ya elimu wa kuwalazimisha wanafunzi kuendelea na masomo katika skuli hizo  na baadae kufanya mtihani wa taifa  katika skuli au kituo chengine.

Mh. Mmanga ameyasema hayo wakati akijibu swali la mwakikishi wa jimbo la mgogoni mh. Sheha hamad,ambae ametaka kujua serikali itachukua hatua gani kwa skuli zote zenye kutekeleza mfumo huo ambao tayari wameshaueleza kwa wanafunzi na wazazi wao.

Wakati huhuo waziri wa ujenzi, mawasikiano,na usafirishaji mh. Dr. Sira ubwa mamboya, amesema jumla ya shilingi bilioni ishirini  zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa meli ya mafuta na meli ya abiria na mizigo.

Akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la kiwani mh. Mussa foum,dr.sira amesema kwa hatua ya awali serikali imeamua kuanza na meli ya mafuta na tayari imeshalipa asilimia 30 ya gharama ya utengenezaji wa meli hiyo.

Mapema serikali kupitia wizara ya nchi ofisi ya makamu wa pili wa rais imesema inathamini jitihada zibazochukuliwa na asasi zisizo za kiserikali ikiwemo zapha+ katika kusaidia mapambano dhidi ya ukimwi.

Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri wa wizara hiyo mh. Mihayo juma nunga wakati akijibu swali la mh. Omar seif abeid ambae ametaka kujua serikali ina mpango gani wa kuzisaidia jumuiya hizo.

Katika hatua nyengine naibu waziri wa biashara na  viwanda mh. Hassan khamis wakati akijibu swali la nyongeza la mwakilishi wa jimbo la chaani mh. Nadir abdullatif,  amesema  karafuu ya zanzibar ndio ya mwanzo yenye ubora duniani.