HATUA ZAHITAJIKA KUONDOA MZOZO MSIKITI SHURBA

 

Hatua za  haraka zinahitaji  kuchukuliwa  kumaliza mzozo uliopo  kuhusu usimamizi wa msikiti wa  afraaa maarufu msikiti shurba uliopo kidongo chekundu mjini zanzibar.

Zbc imegundua baadhi ya baadhi ya waumini waliopo karibu na msikiti huo wameamua kujitenga na kuacha kutumia kwa shughuli zozote za ibada kwa madai kuwa viongozi wake waliopo hawana ushirikiano na jamii.

Wakielezea hali hiyo baadhi ya  waumini wamedai  kuwa mtu  anae uongoza  hataki ushauri wa aina yeyote ambae pia amekataza kuendelezwa madrasa  katika  msikiti  huo kwa madai ya maslahi.

 

Akithibitisha hilo mwazilishi  wa  madrasa  hiyo  ustaadh ismail rashid amesema anashangazwa  kusitishwa kusomesha madrasa  baada   ya   kutokea wafadhili waliojitolea kutoa  ruzuku  kwa  ajili  ya   kuwasaidia   wanafunzi waliofika zaidi ya mia tatu ambao kwa sasa wamelazimika kusoma katika mazingira magumu.

Zbc ilikutana na mtu   aliejitambulisha   kuwa   imamu wa msikiti huo    suleiman abubakari na kukiri kuwepo   kwa mzozo huo lakini hakuwa tayari   kusema chochote kwa madai kuwa yeye si msemaji   wa  msikiti huo.

Jumuiya ya maimanu zanzibar wamekiri kuwepo kwa mzozo katika msikiti huo kufuatia mfadhili aliyeujenga msikiti huo na kuahidi kufuatilia zaidi ilikuweza kusadiana taasisi husika katika kuutatua.

Hata hivyo ameafahamisha kuwa malalamiko mingi inayoibuka ndani ya misikiti inachangiwa zaidi za wananchi kwa ajili ya taama ya maslahi ya kiuchumi au kibinafsi.