HAWAII IMEFANYIA JARIBIO KING’ORA CHA KUONYA SHAMBULIZI LA NYUKLIA.

Hatua hiyo ni mara ya kwanza kufanyika tangu kumalizika vita baridi katika jimbo la hawaii nchini marekani limefanyia jaribio king’ora cha kuonya kuhusu shambulizi la nyuklia
Kufanyika zoezi hiloinatokana na jaribio la kombora la masafa marefu lililofanywa na korea kaskazini mapema wiki hii.
Hawai kawaida ina ving’ora ambavyo huonya kuhusu majanga ya asili kama tsunami tofauti na kingora cha nyuklia ambacho mlio wake huwaonya watu kusalia manyumbani wakisubiri ushauri zaidi.
Kombora linalorushwa kutoka korea kaskazini linaweza kushambulia hawaii ndani ya dakika 20 baada ya kufyatuliwa.
Hivi majuzi korea ilifyatua kombora mpya la masafa marefu ambalo inadai kuwa linaweza kushambulia ndani ya marekani.