HESHIMA YA KIPEKEE KWA KAMPUNI UHANDISI WA UJENZI YA {CCECC} KUTOKA CHINA

 

 

Rais wa kampuni ya kimataifa ya uhandisi wa ujenzi ya  {ccecc} kutoka china  zhuang  shangbiao amesema hatua ya serikali ya mapinduzi ya zanzibar kuwapa kazi ya ujenzi wa bara  bara nchini kimeleta heshima ya kipekee kwa kampuni hiyo.

Amesema jukumu lililopo kwa uongozi na wahandisi wa kampuni hiyo ni kujipanga vyema kuhakikisha heshima waliyopewa na smz wanailinda katika kuwajibika ipasavyo wakati wa utekelezaji wa jukumu hilo zito katika misingi ya ari na bidii kubwa.

Bwana Zhuang  Shangbiao akiuongoza Ujumbe wa Viongozi 7 wa Taasisi hiyo ya Civil Engineering Construction Corporation amesema hayo wakati akitoa shukrani katika mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.

Amesema kasi ya Ujenzi iliyokuwa nayo Kampuni hiyo ya CCECC kwa zaidi ya Miaka 50 iliyopita inahamishiwa Zanzibar  katika Ujenzi wa Bara bara inayoanzia Bububu, Mahonda  kupitia  Kinyasini hadi Mkokotoni yenye urefu wa Kilomita 31.

Bwana Zhuang alimthibitishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Wahandisi wa Ujenzi wa Kampuni ya CCECC watakamilisha kazi hiyo kwa wakati na katika kiwango kinachokubalika Kimataifa kwa vile wana utaalamu na uzoefu wa kutosha.

Rais huyo wa Kampuni ya CCECC alieleza kuwa amesema CCECC yenye utaalamu mkubwa iko tayari pia kuwekeza katika miradi ya ujenzi wa Nyumba za Makaazi na biashara sambamba na kuitikia wito wa uanzishaji wa Viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya uvuvi wa Bahari Kuu utakaotoa ajira pana zaidi kwa Vijana.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Kampuni za Kichina zinastahiki kupongezwa  kutokana na bidii kubwa ya Wahandisi wake katika ujenzi wa Miundombinu tofauti hapa Nchini.

Balozi Seif amesema takwimu zinaonyesha wazi kwamba hivi sasa Kampuni za Kichina zinaongoza kwa kuaminiwa kupewa miradi mbali mbali ya Ujenzi katika Taasisi tofauti za Umma na hata zile Binafsi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimueleza Rais huyo wa Kampuni ya CCECC kwamba kukamilika kwa Ujenzi wa Bara bara hiyo ya Bububu, Mahonda kupitia Kinyasini hadi Mkokotoni kutasaidia kuleta matumaini makubwa kwa Wananchi waliowengi.

Bububu, Mahonda kupitia Kinyasini hadi Mkokotoni  ni Moja ya miongoni mwa Mradi wa Ujenzi wa Bara bara Nne za Unguja uliotiwa saini mnamo Tarehe 8 Novemba Mwaka 2017 hapo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “A” Mkokotoni na kushuhudiwa pia na Makamau wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Mradi huo unaojumuisha pia Bara  bara za Pale  – Kiongele, Matemwe – Muyuni pamoja na Fuoni – Kombeni zinazotarajiwa kuwa na Urefu wa Kilomita 52 unagharamiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  kupitia Mkopo nafuu wa fedha wa shilingi Bilioni 58 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika {ADB}.