HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI WA ZANZIBAR.

 

Wizara ya afya zanzibar na hospitali ya taifa ya muhimbili imetiliana saini mkataba  ya kuwapeleka wagonjwa kutibiwa katika hospitali hiyo, ikiwa na lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi wa zanzibar.

Akizungumza katika hafla hiyo, iliyofanyika wizarani mnazimmoja, mkurugenzi mkuu wa afya zanzibar, dr. Jamala adam taibu, amesema, mkataba huo utaweza kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi ambao walikuwa wakiupata nje ya nchi.

Amesema wizara mara nyingi imekuwa ikipeleka wagonjwa wake hospitali za nje ya nchi ila kusainiwa mkataba huo utaweza kurahisisha matibabu sambamba na kuziokoa fedha zilizokuwa zikitumika wanapopeleka wagonjwa huko.

Nae mkurugenzi mtendaji wa hospitali ya muhimbili, profedha lawrence museru, amesema kuwa mkataba huo unaonesha nia ya kuendelea kushirikiana katika utoaji wa huduma za afya kwa wananchi ndani ya mipaka ya tanzania kwani upelekaji wa mgonjwa nje ya nchi inachukua harama kubwa.

Aidha amesema kuwa wizara imekuwa ikiwekeza katika rasilimali watu pamoja na kuwekeza kutoa huduma kwa usalama na kwa kiwango kinachokubalina, hivyo wagonjwa watakaopelekwa katika hospitali hiyo wataweza kupata huduma iliyokuwa bora.