HOSPTALI BINAFSI ZIMEFUNGIWA KUENDESHA SHUGHULI ZAKE NA BODI YA UKAGUZI

Hosptali nyengine binasf zimefungiwa kuendesha shughuli zake na bodi ya ukaguzi kutokana na kutotimiza masharti ya serikili juu ya uendeshaji wa hospitali hizo.
Hospitali hizi za mkoa wa kaskazini unguja zimechukuliwa hatua hiyo na bodi ya ukaguzi wa hosptali binafsi wakati ilipoendelea na zoezi la ukaguzi ili kuona kama zinafanya kazi vizuri kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa.
Karibu miezi miwili iliyopita bodi hiyo ilizifungia hospitali binafsi nne zote za mkoa wa mjini magharibi ikiwemo ya michenzani, zuha ya fuoni, almajid, alaghalam na koani.
mratibu wa bodi ya ukaguzi wa hospitali binafsi ndugu khamis haji makame amesema wamiliki wote wa hospitali binafsi watakaokwenda kinyume na masharti watakuchukuliwa hatua