HUDUMA YA KWANZA KWA WAFANYAKAZI NI MUHIMU

 

Mwenyekiti wa tume ya kurekebisha sheria jaji mshibe ali bakar amesema huduma ya kwanza kwa wafanyakazi wanaopata  matatizo ya afya ni muhimu kabla ya kufikishwa hospitali kwa matibabu.

Jaji mshibe amesema bado baadhi ya wananchi wanashindwa kufahamu umuhimu wa kujifunza njia sahihi  au kutoa huduma linapotokea tatizo au maafa.

Amesema ni vyema sasa wafanyakazi wa taasisi za umma kupatiwa mafunzo ili kufahamu  namna ya kutoa huduma ya mwanzo yanapotokea maafa  ,ajali au ugonjwa wa hafla maofisini.

Mwenyekiti huyo amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya huduma ya kwanza kwa wafanyakazi wa tume yake huko weles ukumbi wa watu wenye ulemavu.

Akitoa mafunzo hayo mratibu wa redcross zanzibar ubwa suleiman  amesema huduma ya kwanza imegawika sehemu tofauti na kila mtu ana  wajibu wa kujifunza ili kuokoa maisha.