HUDUMA YA MKOBA WA VIFAA KWA MAMA WAJAZITO YAZINDULIWA

 

Wizara ya afya imezindua huduma ya mkoba wa vifaa kwa mama wajazito watakaojifungulia hospitali na vituo vya afya kwa lengo la kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi

Kutokana na ongezeko la vifo vya mama wajawazito mpango huo umelenga moja kwa moja kuwashajihisha wajawazito kutumia hospital na vituo hivyo na kuacha mazoea ya kuzjifungulia nyumbani.

Akizindua huduma hiyo waziri wa afya mh. Hamad rashid mohamed amesema wizara haitosita kumchukulia hatua mtendaji au muuguzi watakaobanika kuuza mikoba hiyo ambayo inatolewa bure kwa wajawazito wanaojifungulia hospitali na vituo vya afya pekee.

Mwakilishi kutoka kwa washirika wa maendeleo  mariyam seif  amesema uzinduzi wa mkoba huo utaweza kupunguza vifo vya akina mama na watoto na kutoa mwamk o kwa akinamama wengine kujifungua katika vituo vya afya.

Katika hatua nyengine kaimu meneja kutoka bohari kuu ya dawa tanzania maco masal amesema upatikanaji wa dawa katika bohari ya dawa ya tanzania na zanzibar umezidi kuongezeka dawa nyingi zinazohitajika kwa wananchi zinapatikana  katika vituo vya afya.

Aidha amefamisha kuwa huduma za mkoba wa vifaa kwa mama wajazito zitakuwa ni za kudumu kwa vifaa hivyo viko vya kutosha na vitagawiwa kwa vituo vyote vya afya tanzania bara na zanzinar.

Naibu katibu mkuu wizara ya afya halima maulid salum, amewataka wafanyakazi wa vituo vya afya kuhakikisha kuwa mkoba huo unatolewa bila malipo yoyote na kila mwananchi aipate huduma hiyo anapofika kituo cha afya wakati wa kujifungua.