HUJUMA ZA ANGANI ZINAENDELEA DHIDI YA MJI MKUU WA YEMEN

Hujuma za angani zinaendelea dhidi ya mji mkuu wa yemen-sanaa- ambazo zimelengwa karibu na uwanja wa ndege pamoja na wizara ya mambo ya ndani ya mjini sanaa.
Ushirika wa kijeshi unaoongozwa na saudi arabia ndio unaohusika na mashambulizi hayo ya angani dhidi ya mji mkuu huo.
Mapigano yanaendelea kati ya wafuasi wa rais wa zamani wa yemen, ali abdullah saleh na washirika wake wa zamani, na wanamgambo wa kishia wa houthi, katika maeneo ya nje ya mji mkuu sanaa.
Mwishoni mwa wiki ali abdullah saleh alitoa wito kwa nchi washirika zinazoongozwa na saudi arabia zisitishe mashambulizi yao na kusema kuwa yupo tayari kwa mazungumzo na viongozi wa mjini riyadh.