HUJUMA ZA KUCHOMA MOTO MASHAMBA YA MIWA KATIKA KIWANDA CHA SUKARI MAHONDA ZIMEPUNGUA

Waziri wa nchi afisi ya rais tawala za mikoa na idara maalum za smz mhe, haji omar kheri amesema hujuma za kuchoma moto mashamba ya miwa katika kiwanda cha sukari mahonda zimepungua tokea mashamba hayo kulindwa na kikosi cha valantia.
Amesema kikosi hicho kinalipwa shilingi milioni 11.5 kwa kazi ya kulinda miwa ambayo ni malighafi ya kiwanda hicho kinachoendeshwa na wawekezaji kutoka india.
Akijibu swali katika kikao cha baraza la wawakilishimh kheri amesema kiwanda cha sukari mahonda kinachangia pato la taifa na kutoa ajira kwa vijana
Aidha amesema hivi karibuni .serikali inatarajia kukabidhi uongozi wa kiwanda hicho nyumba zilizojengwa tokea kuanzishwa kiwanda hicho kwa ajili ya makazi ya wafanyakazi.
Wakati huo huo naibu waziri wa ardhi maji ,nishati na mazingira mhe, juma makungu amesema wizara hiyo inahitaji shilingi milioni moja na nusui ili kukamilisha mradi wa kuwapatia maji safi na salama wananchi wa michamvi kutoka katika visiwa viwili vilivyochibwa kwa ajili hiyo.
Katika hatua nyingine naibu waziri wa kazi uwezeshaji wazee, vijana wanawake na watoto mhe, shadia mohammed suleima amesema jumla ya kesi 198 zimeripopiwa mkoa kaskazini pemba kutoka januari 2017 hadi juni 2017 hali inayoonesha kuongezeka kwa tatizo hilo.