IBADA YA SHUKRANI KWA KUKAMILISHA UKARABATI WA KANISA

Waumini wa dini ya kikristo wamehimizwa kutekeleza ibada kwa kumkumbuka muumba wao pamoja na kushukuru kwa wanayobarikiwa katika dunia ikiwemo kujenga maisha yao.
Akitoa mahubiri katika sherehe ya ibada ya shukrani kwa kukamilisha ukarabati wa kanisa la Anglikan Dayosisi ya Zanzibar mkunazini,baba askofu dk.maimbo mndolwa kutoka dayosisi ya tanga amewataka waumini hao kujitathmini wao wenyewe katika suala zima la kufanya ibada kwani ndio malengo ya kuimarisha majengo hayo na kwamba kanisa sio majengo bali ni ibada inayotekelezwa ndani yake ambayo ni moja ya kujenga maisha ya mwanaadmu.
Waziri wa kazi,uwezeshaji wazee,vijana na watoto mh.moudline castico amesisitiza waumini wa dini zote kuendeleza upendo,amani na mshikamano katika nchi ili kuongeza kasi ya maendeleo katika taifa.
Kwa upande wake askofu wa anglikana zanzibar michael hafidh amesema wanaishukuru serikali kwa kuimarisha amani na utulivu nchini lakini bado waumini wa dini ya kikiristo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto katika kutekeleza kwa ufanisi shughuli zao.