IDADI YA WALIOKUFA KUTOKANA NA TETEMEKO LA ARDHI MEXICO IMEFIKIA ZAIDI YA WATU 200

Idadi ya waliokufa kutokana na tetemeko kubwa la ardhi nchini mexico imefikia zaidi ya watu 200, wengi wao wakiwa ni watoto 21 walioangukiwa na shule yao kusini mwa mji mkuu, mexico city.
Mkuu wa idara ya kushughulikia majanga nchini humo, amesema maafisa wa uokozi wanajaribu kuwatafuta manusura wa tetemeko hilo.
Wengi wa walioathirika ni katika mji mkuu, ambako watu 117 waliripotiwa kupoteza maisha, watu wengine 94 wamefariki dunia katika majimbo mengine.
Tetemeko hilo la ardhi, linasadifiana na siku ambayo mexico ilikumbwa na tetemeko kubwa mnamo mwaka 1985 ambapo zaidi ya watu elfu 10 waliuawa.