IDADI YA WANAFUNZI WANAOPEWA UJAUZITO

 

Walimu katika skuli ya unguja ukuu wilaya ya kati wamesema kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaopewa ujauzito kunatokana na baadhi ya wazazi kuendelea kuwalinda wafanyaji wa vitendo hivyo.

Mwalimu mkuu wa skuli hiyo suleiman ali seif wakati mkuu wa mkoa kusini unguja  mhe, hassan khatib hassan alipotembelea skuli hiyo kusikiliza kero zinazowakabili walimu na wanafunzi na kupanga mikakati mipya itakayosaidia kuinua kiwango cha ufaulu katika skuli hiyo.

Amesema kitendo kinachofanywa na baadhi ya wazazi wa wanafunzi cha  kuwalinda wanaowapa ujauzito wanafunzi na wengine kuwatolesha mimba hakikubaliki na kinarejesha  nyuma jitihada za upatikanaji wa maendeleo ya watoto.

Mkuu wa mkoa huo mhe hassan amesema serikali mkoani humo haitasita kuwashughulikia wazazi watakaoshirikiana na wafanyaji wa vitendo hivyo endapo  watabainika wanamaliza kesi hizo katika ngazi ya familia .

Wazazi wa wanafunzi wa skuli  hiyo wamesema matumizi mabaya ya utandawazi, ngoma za mara kwa mara na kuweko kwa nyumba ya ukaba kunachangia kwa kiasi kikubwa kuporomoka kwa maadili kijijini unguja ukuu.

Kikao hicho kilichofanyika skulini hapo kimewashirikisha wazazi, walimu, wanafunzi pamoja na masheha wa shehia tatu za kijiji hicho.