IDADI YA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA INAONGEZEKA SIKU HADI SIKU LICHA YA JITIHADA ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI

Idadi ya watumiaji wa dawa za kulevya inaongezeka siku hadi siku licha ya jitihada zinazochukuliwa na serikali katika kudhibiti utumiaji wa dawa hizo hapa nchini.
Akisoma hoja binafsi ya ongezeko la uingizwaji na utumiaji wa dawa za kulevya zanzibar mjumbe wa baraza la wawakilishi mh’ moh’d said dimwa amesema hali hiyo imekuwa ikileta malalamiko makubwa kwa wananchi juu ya kukithiri kwa rushwa katika shuhuli zote zinazohusiana na dawa za kulevya hasa kwa wasafirishaji.
Amefahamisha kuwa kukithiri kwa vitendo vya rushwa kunawafanya wananchi wengi kukosa imani na vyombo vinavotoa haki ikiwemo jeshi la polisi, afisi ya mwendesha mashtaka (dpp) pamoja na mahkama hali inayopelekea kurudi nyuma juhudi za serikali katika kukabiliana na tatizo hilo.
Mh’ dimwa amesema mbali na kutokea kwa athari juu ya matumizi ya dawa hizo wapo baadhi ya watumiaji wa tanzania na zanzibar ni miatano na sabiini na nane wamekamatwa katika nchi mbali mbali ikiwemo brazil, iran, ethopia na afrika kusini kwa kujihusisha na biashara hiyo, kwa kupatiwa kifungo cha maisha nje ya nnchi na wengine wanasubiria kunyongwa.wakichangia hoja hiyo wajumbe wa wawakilishi wamesema kuwepo kwa utalii kumeonekana kuwa ni njia moja ya wapo ya kuingizwa dawa za kulevya nchini pamoja na kuvisisitiza vyombo vinavyohusika kuzichunguza soba hause zote ili zinazoenda kunyume na taratibu zifungiwe.