IDARA MAALUM ZA SMZ WATAKIWA KUANDAA BAJETI

 

 

Watendaji wa wizara ya ofisi ya Rais tawala za mikoa serikali za mitaa na idara maalum za smz watakiwa kuandaa bajeti zinazozinagatia kuleta maendeleo ya jamii.

Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa serikali mitaa na idara maalum za smz mh. Haji Omar Kheri amesema mabadiliko ya madaraka mikoani yanayofanyika nchini hayawezi kufikia kama hajafikia lengo la kutatua matatizo yanayowakabili wananchi.

Ametoa agizo hilo katika kikao cha kamati ya uongozi wa wizara kilichojadili utendaji ya wizara hiyo ambapo pia ameahidi kusimamia kwa kina utandaji wa wizar hiyo ilikuhakikisha malengo ya serikali yanafikiwa

baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wametoa maoni na mapendekezo ya kufanikisha mipango bora ya bajeti hiyo ya wizara ya nchi ofisi ya rais tawala za mikoa serikali za mitaa na idara maalum za smz ili kufikia lengo.