IDARA YA KILIMO IMEANGAMIZA TANI 28 ZA VITUNGUU SOMU

 

Idara ya kilimo kitengo cha ukaguzi wa mazao na karantin bandarini imeangamiza tani 28 za vitunguu somu ambavyo havifai kwa matumizi ya binaadamu.Akizungumzia vitunguu hivyo kaimu mkuu wa kitengo hicho  bi, hawa suleiman amesema tani hizo za vitunguu vimegundulika october mwaka jana baada ya bwana abdallah said suleiman kuingiza nchini kontena mbili kutoka china.Bi hawa amesema kontena hizo zilikosa baridi na ndio chanzo cha kuharibika kwake.Baadhi ya  walioshiriki katika kuangamiza vitunguu hivyo huko unguja ukuu wamewaonya wananchi kutotumia vitu vinavyothibitishwa kuwa na madhara  kwao..