IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA IMESEMA IMEJIPANGA KUHAKIKISHA SUALA LA WAHAMIAJI HARAMU

Idara ya UhamiajiTtanzania imesemaIimejipanga Kuhakikisha Suala La Wahamiaji haramu wanaoingia Nchini Kinyume na Utaratibu wa Kisheria wa Uhamiaji Wanadhibitiwa.

Tamko hilo limetolewa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anna Peter Makakala wakati Alipotembelea Bandari Ndogo yaMkokotoni Kkaskazini Unguja,ambayo Inatumika Zaidi kwa Wasafiri Kutoka Tanga.

Amesema Ushirikiano Kati ya Wananchi Idara ya Uhamiaji Pamoja na Vyombo Vyengine vya Ulinzi na Usalama Utaongeza Nguvu za Kuweza Kudhibitiwa Wahamiaji Haramu Ambao Baadhi yao Wamekuwa Wakijihusisha ni Vitendo vya Kihalifu.

Akionesha Msisitizo juu ya Udhibiti wa Wageni Wanaoingia Kinyume na Sheria za Uhamiaji, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, Jumanne Tabaran Mzee, Amesema Wamekuwa na Mkakati wa KukabilianaVyema na Hali Hiyo.

Ziara hiyo Imeendelea kwa Kukagua Ofisi za hamiji Kinduni, Uunga Wilaya ya Kati na Ofisi ya Wilaya iliyopo Makunduchi.

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App