IDARA YA UHAMIAJI ZANZIBAR IMESEMA NGUVU ZINAHITAJIKA KUDHIBITI WAHAMIAJI HARAMU

 

Idara ya Uhamiaji Zanzibar imesema nguvu za pamoja zinahitajika kudhibiti wahamiaji haramu ili kuhakikiha hawasababishi maradha kwa wenyeji na kuhatarisha usalama wa nchi.

akitoa  mada katika semina ya uhamiaji haramu iliyofanyika bandari zanzibar ,mrakibu wa uhamiaji  Madina Khalid Hassan  amesema  tatizo la uhamiaji haramu ilimekuwa kubwa ulimwenguni kwa sababu mbali mbali na zanzibar kwa vile ni sehemu ya dunia tatizo hilo pia lipo.

amewataka wanancho wote kuisaidia idara ya uhamiaji kwa kutoa taarifa za kuwabaini wageni wanaowashukia kuwani wahamiaji haramu ili iweze kuchukuwa hatua zinazofaa.

mapema akifunguwa semina hiyo iliyowashirikishwa wandau mbali mbali  wa bandari ya malindi likiwemo shirika la meli,kikosi cha kmkm,zrb,madereva wa tax,kikosi cha zimamoto  na kamisheni ya utalii, afisa uhamiaji mkoa mjini magharibi dc i said hamdani amesema wahamiaji haramu  wanaweza kusababbisha matatizo mengi ikiwa ni pamoja na maradhi ,kuchukuwa ajira za wazalendo na kuhatarisha usalama.