ILI WANAWAKE WAFANIKIWE KIBIASHARA NI LAZIMA KUWA NA LENGO MOJA WAKATI WANAPOFANYA BIASHARA ZAO.

 

Makamo mwenyekiti wa jumuiya ya watoa huduma. Mafuta na gesi tanzania bw. Abdulrahim amesema ili wanawake wafanikiwe kibiashara ni lazima kuwa na lengo moja wakati wanapofanya biashara zao.Amesema bila ya kuwa na lugha moja malengo wanayokusudia hayawezi kufikiwa.

Akifunga  mafunzo kwa wajasilia mali wadogo wadogo  makamo mwenyekiti huyo amesema watu wengi wanashindwa  kukuza uchumi wao kutokana na uvivu na kutokuwa na malengo.Akizungumzia mafunzo hayo mwazilishi wa kampeni ya mwanamke chakarika abla moh’d bakar amesema  mafunzo  hayo yamehusiana na kuwajengea uwezo na kufahamu masoko.Awali amina kheir amesema mafunzo yamelenga  wanawake wote hadi vijijini na ifikapo 2030 wanawake wote waweze kujitegemea kiuchumi.